Mtu afanye nini ikiwa hakumbuki ni siku ngapi alikula Ramadhaan?

Swali: Nilikula Ramadhaan kutokana na udhuru na nikawa na shaka ni idadi ngapi nilizokula. Nifanye nini?

Jibu: Chukua idadi ya chini. Ikiwa ulikula kutokana na udhuru katika Ramadhaan na hujui ni idadi ya siku ngapi ulikula, chukua idadi ya chini. Ikiwa unawekea shaka juu ya kwamba nilikula siku tatu au nne, jaalia iwe siku tatu. Chukua idadi ya chini. Kwa nini? Kwa sababu katika hali hii asli ni kutokula. Maadamu hujakuwa na uhakika juu ya kwamba ulikula siku nne, haikulazimu kitu isipokuwa kile ulicho na yakini nacho ambacho ni siku tatu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kanda “Liqaa´aatu Ramadhwaaniyyah”, sehemu ya 03
  • Imechapishwa: 23/09/2020