Mtindo wa kuzigawa nywele kwa upande mmoja

Swali 1456: Ni ipi hukumu ya kugawa nywele kwa upande mmoja na kuzifuma kuwa mkia mmoja tu kwa lengo la kujipamba kwa ajili ya mume wake au kuonekana kwa mwonekano unaofaa?

Jibu: Ama kugawa nywele kwa upande mmoja, hilo ni kujifananisha na wanawake makafiri. Imethibiti kwamba kujifananisha na makafiri ni haramu kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama kuzifuma kuwa msuko mmoja au zaidi na kuziacha nyuma yake zikiwa zimesukwa au bila kusukwa, hakuna tatizo katika hilo muda wa kuwa zimefunikwa.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/183)
  • Imechapishwa: 29/10/2026