Swali 5007: Je, inajuzu kwa mwanamke kukata nywele zake kwa mujibu wa Shari´ah?

Jibu: Haijuzu kwake kukata au kunyoa nywele za nyusi zake au nywele za kichwa chake isipokuwa kwa dharurah inayopelekea kufanya hivyo, kama kutibu majeraha ya kichwa au nyusi ambazo matibabu yake yanategemea kukata nywele au sehemu yake. Katika hali hiyo inajuzu kufanya hivyo kwa kiwango cha haja tu. Ni lazima kwake kuondoa nywele za usoni mwake na sehemu nyingine zote za mwili wake kwa kuzinyonyoa, kutumia dawa ya kuondoa nywele au mfano wake, isipokuwa nywele za kichwa na nyusi.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/183)
  • Imechapishwa: 29/10/2026