Tunamwambia msomaji mpendwa – mwenye kutafuta haki – kuwa sasa imedhihirika wazi hila na madai ya uongo dhidi ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na kwamba mtindo huu wa kuwazulia watu kauli ambazo hawajasema ni njia inayojulikana sana kwa watu wa Bid´ah. Hawajali juu ya kudhulumu au kuzua uongo alimradi tu yanahimiza wanachokitaka, jambo ambalo linapingana moja kwa moja na maamrisho ya Allaah katika Kitabu Chake na yale aliyoamrisha Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Sunnah yake. Allaah ameamrisha uadilifu na amekataza dhuluma. Hayo vilevile yamebainishwa na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ummah wake. Allaah amesema:
وَمَن يَكْسِبْ خَطِيئَةً أَوْ إِثْمًا ثُمَّ يَرْمِ بِهِ بَرِيئًا فَقَدِ احْتَمَلَ بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا
”Na atakayechuma kosa au dhambi kisha akamtupia asiye na hatia, basi kwa hakika amejitweka usingiziaji na dhambi ya wazi.”[1]
Ni dhambi ipi kubwa zaidi kuliko kumzulia mtu maneno ambayo hajawahi kuyasema?
[1] 04:112
- Muhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 253-254
- Imechapishwa: 11/09/2026
Tunamwambia msomaji mpendwa – mwenye kutafuta haki – kuwa sasa imedhihirika wazi hila na madai ya uongo dhidi ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na kwamba mtindo huu wa kuwazulia watu kauli ambazo hawajasema ni njia inayojulikana sana kwa watu wa Bid´ah. Hawajali juu ya kudhulumu au kuzua uongo alimradi tu yanahimiza wanachokitaka, jambo ambalo linapingana moja kwa moja na maamrisho ya Allaah katika Kitabu Chake na yale aliyoamrisha Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Sunnah yake. Allaah ameamrisha uadilifu na amekataza dhuluma. Hayo vilevile yamebainishwa na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa ummah wake. Allaah amesema:
وَمَن يَكْسِبْ خَطِيئَةً أَوْ إِثْمًا ثُمَّ يَرْمِ بِهِ بَرِيئًا فَقَدِ احْتَمَلَ بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا
”Na atakayechuma kosa au dhambi kisha akamtupia asiye na hatia, basi kwa hakika amejitweka usingiziaji na dhambi ya wazi.”[1]
Ni dhambi ipi kubwa zaidi kuliko kumzulia mtu maneno ambayo hajawahi kuyasema?
[1] 04:112
Muhusika: ´Allaamah ´Aliy bin Naaswir al-Faqiyhiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ar-Radd al-Qawiym, uk. 253-254
Imechapishwa: 11/09/2026
https://firqatunnajia.com/mtindo-mchafu-wa-wazushi-wote/