Swali: Mtu aliyepo Haram hakuwezi kuiona Ka´bah na hivyo akaelekea kama waswaliji wengine. Baada ya kumalizika kuswali ikambainikia kuwa hakuelekea katika Ka´bah yenyewe. Ni ipi hukumu ya swalah yake?
Jibu: Ikiwa hawakufanya itjihada yao ya mwisho, basi naona kuwa ni lazima wairudie swalah yao. Kimsingi ni kwamba mtu anaweza kufanya ijtihada yake ya mwisho kabisa. Hata kama yuko mahali ambapo haioni Ka´bah wanaposimama watu, basi kuna uwezekano akaiona. Hata hivyo kunaweza kusemwa kwamba mtu kama huyo ni mwenye kupewa udhuru katika hali kama hiyo, hapo ni pale atapokuja na watu wamekwishaanza kuswali na safu yake iko kwa mbali ambapo inakuwa ni vigumu sana kwake kuiona Ka´bah na pengine isiwezekane hata kuiona Ka´bah yenyewe, katika hali hiyo inatosha kuelekea upande wa Ka´bah kutokana na ugumu.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/411-412)
- Imechapishwa: 10/04/2026
Swali: Mtu aliyepo Haram hakuwezi kuiona Ka´bah na hivyo akaelekea kama waswaliji wengine. Baada ya kumalizika kuswali ikambainikia kuwa hakuelekea katika Ka´bah yenyewe. Ni ipi hukumu ya swalah yake?
Jibu: Ikiwa hawakufanya itjihada yao ya mwisho, basi naona kuwa ni lazima wairudie swalah yao. Kimsingi ni kwamba mtu anaweza kufanya ijtihada yake ya mwisho kabisa. Hata kama yuko mahali ambapo haioni Ka´bah wanaposimama watu, basi kuna uwezekano akaiona. Hata hivyo kunaweza kusemwa kwamba mtu kama huyo ni mwenye kupewa udhuru katika hali kama hiyo, hapo ni pale atapokuja na watu wamekwishaanza kuswali na safu yake iko kwa mbali ambapo inakuwa ni vigumu sana kwake kuiona Ka´bah na pengine isiwezekane hata kuiona Ka´bah yenyewe, katika hali hiyo inatosha kuelekea upande wa Ka´bah kutokana na ugumu.
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/411-412)
Imechapishwa: 10/04/2026
https://firqatunnajia.com/mswaliji-haram-haioni-kabah/