Mswaliji anayeswali peke yake baadaye kuwa imamu

Swali: Je, inasihi kwa mtu anayeswali peke yake kuwa imamu katika swalah ya faradhi?

Jibu: Ndio, inasihi kwa mtu anayeswali peke yake kuwa imamu, ni mamoja katika swalah ya faradhi au inayopendeza. Dalili ya hilo ni kwamba siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama usiku mmoja kuswali. Ibn ´Abbaas naye akasimama na kusimama upande wa kushotoni mwake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akanivuta kwa nyuma yake na kuniweka upande wa kuliani mwake[1]. Yale yaliyothibiti katika swalah inayopendeza yanathibiti pia katika swalah ya faradhi isipokuwa kama dalili inaonyesha kinyume.

Ikiwa maamuma ndiye msafiri na imamu ni mkazi – je, inafaa kwa msafiri kumaliza swalah kivyake baada ya kumaliza kuswali Rak´ah mbili? Hapana. Maamuma ambaye ni msafiri anaposwalishwa na imamu mkazi haifai kwake kumaliza swalah kivyake baada ya kumaliza kuswali Rak´ah mbili. Kwa sababu maamuma msafiri akiswalishwa na imamu ambaye ni mkazi basi ni lazima kwake kuswali kwa kukamilisha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika hapana vyengine imamu amewekwa ili afuatwe.”[2]

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kile mnachowahi swalini, na kile kilichokupiteni kamilisheni.”[3]

[1] al-Bukhaariy (183).

[2] al-Bukhaariy (722) na Muslim (417).

[3] al-Bukhaariy (636) na Muslim (602).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/450-451)
  • Imechapishwa: 19/03/2026