Msimamo wa Raafidhwah juu ya misikiti

Raafidhwah wana msimamo wa kuchupa mipaka kwa Mitume bali mpaka kwa maimamu. Wameenda mbali mpaka wamefikia kuwafanya kuwa ni washirika wa Allaah. Wameenda kinyume na Mitume na wakaacha kumwabudu Allaah pekee. Wamemkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa yale aliyowakhabarisha juu ya kutubia kwa Manabii na kuomba kwao msamaha.

Matokeo yake utawaona namna wanavyoiepuka misikiti ambayo Allaah kaamrisha litukuzwe ndani yake jina Lake. Hawaswali ndani yake si swalah ya ijumaa wala swalah ya mkusanyiko. Misikiti haina heshima kubwa katika maisha yao. Hata wakifanya hivo, basi kila mmoja anaswali kivyake.

Badala yake wanaadhimisha makuba yaliyojengwa juu ya makaburi. Wanabaki hapo kwa muda mrefu kama wafanyavyo washirikina. Wanahiji kwenda huko kama anavyohiji mwenye kuhiji kwenda katika Ka´bah. Wako ambao wanaona kuhiji kwenye makaburi ni jambo kubwa kuliko kuhiji kwenda katika Ka´bah. Bali wanamtukana yule ambaye ametosheka na ile hajj aliyofaradhishiwa na Allaah na swalah ya ijumaa na swalah ya mkusanyiko.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/474)
  • Imechapishwa: 29/01/2019