Swali: Ni ipi hukumu ya kuwa na mapenzi na mtu ambaye haswali isipokuwa swalah ya ijumaa peke yake? Je, inafaa kumkata ikiwa hilo linaidhuru familia?

Jibu: Tunaposema kuwa mtu hakufuru isipokuwa kwa kuacha swalah kabisa, ina maana kwamba huyu anayeswali ijumaa peke yake hakufuru. Kwa sababu hakuacha swalah kabisa. Na tukisema kuwa anakufuru kwa kuacha swalah moja tu au mbili zinazoweza kukusanywa pamoja, basi mtu huyu anakuwa kafiri. Wakati tunapomuhukumu kuwa ni kafiri basi ni lazima kumkata na kumsusa. Bali ni wajibu kumtaka atubie; akitubia ni sawa na vinginevyo anauliwa[1].  Lakini tukisema kuwa sio kafiri, basi kumkata kutategemea na manufaa na madhara. Tukiona kuwa manufaa ni kule kumsusa, basi tutamtusa, na tukiona kuwa hakuna manufaa kufanya hivo, basi hatotumkata.

[1] Zayd al-Madkhaliy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Si haki ya kila mmoja kusimamisha adhabu za Kishari´ah. Isipokuwa yule aliyetawalia madaraka ya waislamu. Mtawala wa Kiislamu ndiye mwenye haki ya kusimamisha adhabu kama vile ya kumuua anayeua makusudi, anakata mkono wa mwizi, anampiga bakora mzinzi ambaye hajawahi kuingia ndani ya ndoa, atampiga mawe mzinzi ambaye kishawahi kuingia ndani ya ndoa na atampiga mijeledi mtu ambaye anawatuhumu wengine machafu na mnywaji pombe.” (at-Ta´liyqaat al-Latwiyfah ´alaa Usuwl-is-Sunnah al-Muniyfah, uk. 116-118)

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/110)
  • Imechapishwa: 12/04/2026