Swali: Bwana huyu kazini daima anamsambazia shubuha. Shubuha ya kwanza anasema kuwa ”lau” inafungua mlango wa shaytwaan ilihali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Lau nisingechelea kuwatia uzito ummah wangu basi ningewaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah.”[1]

Daima ni kwamba anamuenezea hoja tata. Amfanye nini?

Jibu: Amwache na amwambie asizungumze naye.

Mwanafunzi: Amuhame?

Ibn Baaz: Ikiwa anamwambia kitu kinachomuudhi amwambie asiongee naye.

Mwanafunzi: Anasema kuwa ”lau” inafungua mlango wa shaytwaan ilihali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Lau nisingechelea kuwatia uzito ummah wangu basi ningewaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah.”

Ibn Baaz: Shubuha iko wapi sasa?

Mwanafunzi: Mtume ndiye amesema hivo.

Ibn Baaz: Kuna nini sasa?

Mwanafunzi: Anachokusudia ni kwamba amekataza watu kusema ”lau” kisha yeye mwenyewe ametumia lau katika Hadiyth hapo juu?

Ibn Baaz: Hapana, hayo ni mambo mawili tofauti. Makatazo ya lau ni wakati mtu anapofikwa na kile alichoandikiwa ndipo anasema ”lau ningelifanya kadhaa… ”, ”lau ningelimwendea daktari ingelikuwa kadhaa” au ”lau ningelisafiri ingelikuwa kadhaa”. Haya ndio yamekatazwa. Badala yake anatakiwa kusema:

قدر الله وما شاء فعل

“Qadar ya Allaah; akitakacho huwa.”

Hili haluhusiani na Hadiyth isemayo:

”Lau nisingechelea kuwatia uzito ummah wangu basi ningewaamrisha kutumia Siwaak wakati wa kila swalah.”

Kwa maana ya kwamba ingelikuwa sio ule uzito utaowapata angelifanya hivo. Hiyo ni rehema ya Allaah kwa waja. Hakuna mgongano kabisa.

Mwanafunzi: Kwa hiyo ahamwe?

Ibn Baaz: Hapana, anamfundisha na kumuelekeza.

[1] al-Bukhaariy (887) na Muslim (252).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24677/حكم-مخالطة-مثيري-الشبهات
  • Imechapishwa: 24/11/2024