Swali: Ikiwa nina jamaa wasioswali na wanafanya maovu majumbani kwao kama kuchanganyika bila mipaka na mengineyo, nami siwezi kuwakaripia – Je, ni wajibu kwangu kuwatembelea?

Jibu: Ikiwa ndugu zako wanatenda maovu, una jamaa wanaofanya maovu, basi una hali mbili: ima uwaunge kwa ajili ya kuwakanya na kuwapa nasaha, jambo ambalo ni jema. Unawatembelea kwa ajili ya kukanya na kuwanasihi. Wakiitikia ni vyema, na wakibaki katika batili yao basi unawaacha na huwazuru. Kwa sababu hawastahiki kutembelewa muda wa kuwa wako juu ya maovu ya wazi kama kunywa pombe, kuacha swalah au mfano wa hayo katika maasi ya wazi. Kuacha swalah ni ukafiri mkubwa kuliko madhambi makubwa. Hivyo mwenye hali hii, anayetenda maovu haya ya kuacha swalah na kunywa vilevi, huyu hatembelewi isipokuwa kwa ajili ya nasaha. Ikiwa nasaha inamfaa, basi atembelewe na apewe nasaha na aelekezwe katika kheri. Akiitikia, ni jambo jema, na asipoitikia aachwe na asitembelewe tena. Ahame mpaka Allaah amuongoze baadaye.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/992/حكم-هجر-من-يجاهر-بالمعاصي-من-الاقارب
  • Imechapishwa: 24/12/2025