Swali: Msichana wangu amekufa akiwa na miaka 13. Je, analazimika kuhiji?

Jibu: Kama alikuwa amekwishabaleghe, akawa na uwezo na yuko pamoja na Mahram basi hajj inamuwajibikia. Lakini kama alikuwa hajabaleghe, alikuwa hana mali au alikuwa hana Mahram basi kimsingi hajj haimlazimu.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Khaatam-ul-Mursaliyn https://godian.af.org.sa/sites/default/files/2017-10/lqa-mftoh-godian.mp3
  • Imechapishwa: 27/09/2022