Swali: Mimi ni kijana nina cheti cha kanuni au sekondari ya kimarekani kilichothibitishwa na Wizara ya elimu. Lakini mmoja wa marafiki zangu ndiye aliyefanya mtihani kwa niaba yangu. Cheti hiki kimethibitishwa kwa ajili ya kazi nchini Saudi Arabia, si kwa ajili ya masomo, bali kazi tu. Ni ipi hukumu ya mshahara ninaoupokea kutokana na kazi hii? Je, mshahara huu unahusiana na cheti au na kazi ninayoifanya?
Jibu: Hili ni kosa kubwa na halijuzu. Hili ni katika kughushi na kusema uongo na kula mali isiyokuwa kwa haki yake. Uliwasilisha cheti ambacho si chako na kilichoghushiwa kwa ajili yako, jambo ambalo halijuzu wala halihalaliki. Ni wajibu juu yako kutubia kwa Allaah kutokana na hilo, kuacha kazi hii mbaya na kutafuta ajira kwa njia nyingine za kweli kutoka kwako mwenyewe, kama kuonyesha kuwa umefanya kazi fulani na fulani na kuwa umefaulu katika kazi yako ili upate cheti kutoka kwa wale wanaojua kazi yako, juhudi zako na bidii yako katika kazi. Ama cheti hiki kilichoghushiwa, usikitoe kwa watu. Na ni juu yako kutubia kwa Allaah kutokana na yaliyopita. Ikiwa ulikuwa unafanya kazi uliyopewa na ukaitekeleza ipasavyo na hukufanya khiyana ndani yake, bali uliitekeleza haki yake na ukafaulu, basi unastahiki yale uliyopewa kwa kazi yako. Lakini ni juu yako kutubia kwa Allaah kutokana na ule udanganyifu ulioutanguliza.
Swali: Je, ni lazima awaambie waajiri?
Jibu: Hapana, lakini ni juu yake kutubia kwa Allaah.
Swali: Anaweza kuchukua mshahara alioupata hapo awali?
Jibu: Ni juu yake kutubia kwa Allaah na huo mshahara ni kutokana na kazi yake aliyofanya.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3332/حكم-الراتب-المستلم-من-العمل-والمتعلق-بشهادة-مزورة
- Imechapishwa: 29/09/2026
Swali: Mimi ni kijana nina cheti cha kanuni au sekondari ya kimarekani kilichothibitishwa na Wizara ya elimu. Lakini mmoja wa marafiki zangu ndiye aliyefanya mtihani kwa niaba yangu. Cheti hiki kimethibitishwa kwa ajili ya kazi nchini Saudi Arabia, si kwa ajili ya masomo, bali kazi tu. Ni ipi hukumu ya mshahara ninaoupokea kutokana na kazi hii? Je, mshahara huu unahusiana na cheti au na kazi ninayoifanya?
Jibu: Hili ni kosa kubwa na halijuzu. Hili ni katika kughushi na kusema uongo na kula mali isiyokuwa kwa haki yake. Uliwasilisha cheti ambacho si chako na kilichoghushiwa kwa ajili yako, jambo ambalo halijuzu wala halihalaliki. Ni wajibu juu yako kutubia kwa Allaah kutokana na hilo, kuacha kazi hii mbaya na kutafuta ajira kwa njia nyingine za kweli kutoka kwako mwenyewe, kama kuonyesha kuwa umefanya kazi fulani na fulani na kuwa umefaulu katika kazi yako ili upate cheti kutoka kwa wale wanaojua kazi yako, juhudi zako na bidii yako katika kazi. Ama cheti hiki kilichoghushiwa, usikitoe kwa watu. Na ni juu yako kutubia kwa Allaah kutokana na yaliyopita. Ikiwa ulikuwa unafanya kazi uliyopewa na ukaitekeleza ipasavyo na hukufanya khiyana ndani yake, bali uliitekeleza haki yake na ukafaulu, basi unastahiki yale uliyopewa kwa kazi yako. Lakini ni juu yako kutubia kwa Allaah kutokana na ule udanganyifu ulioutanguliza.
Swali: Je, ni lazima awaambie waajiri?
Jibu: Hapana, lakini ni juu yake kutubia kwa Allaah.
Swali: Anaweza kuchukua mshahara alioupata hapo awali?
Jibu: Ni juu yake kutubia kwa Allaah na huo mshahara ni kutokana na kazi yake aliyofanya.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3332/حكم-الراتب-المستلم-من-العمل-والمتعلق-بشهادة-مزورة
Imechapishwa: 29/09/2026
https://firqatunnajia.com/mshahara-anaopata-mtu-kwa-cheti-feki/