Msafiri amemaliza swalah yake baada ya kuwahi Rak´ah mbili nyuma ya mkazi

Swali: Mtu amejiunga katika swalah akiwa msafiri na akaswali nyuma ya imamu anayeswali swalah ya ´Aswr, hakuwahi isipokuwa Rak´ah mbili tu. Naye msafiri alikuwa amenuia kuswali kwa kufupisha. Akaswali Rak´ah hizo mbili pamoja na imamu kisha akasalimu pamoja naye. Ni ipi hukumu ya swalah yake?

Jibu: Msafiri akiswali nyuma ya mkazi huswali Rak´ah nne. Sunnah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwamba aswali Rak´ah nne akimfuata mkazi. Hivyo aliyewahi Rak´ah mbili za mwisho na akaziswali pamoja na mkazi, inamlazimu kuongezea Rak´ah mbili baada ya mkazi kusalimu ili kukamilisha nne. Yule ambaye hakufanya hivyo, basi inampasa kuirudia swalah aliyoswali Rak´ah mbili tu, kwa sababu kwake ni wajibu kuswali Rak´ah nne akiwa nyuma ya mkazi. Msafiri akiswali nyuma ya mkazi, huswali pamoja naye Rak´ah nne.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31700/هل-يتم-المسافر-الصلاة-اذا-صلى-مسبوقا-مع-مقيم
  • Imechapishwa: 15/11/2025