Msafiri amedema katika kituo na mji wake ilihali amefunga

Swali: Msafiri amedema katika kituo chake. Je, safari yake imekatika?

Jibu: Safari ya msafiri haikatiki kwa sababu tu amedema katika kituo chake. Inajuzu kwake kuendelea kuacha kufunga katika Ramadhaan hata kama atabaki hivo mwezi mzima. Ama akirudi katika nchi yake hali ya kuwa si mwenye kufunga, sio wajibu kwake kufunga siku iliyobaki. Inafaa kwake kula na kunywa siku iliyobaki. Kufunga siku iliyobaki hakuna maana yoyote kwa vile kwa vovyote atailipa siku hii. Haya ndio maoni sahihi na ni maoni vilevile ya Maalik, ash-Shaafi´iy na Ahmad (Rahimahumu Allaah) katika moja ya mapokezi yake. Hata hivyo asile na kunywa hadharani.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/99)
  • Imechapishwa: 30/05/2017