Swali: Kuna mposaji kamchumbia mwanamke. Wakati alipouliza juu yake ikabaini kuwa haswali. Je, amuozeshe bwana huyu?
Jibu: Ikiwa mposaji haswali swalah ya mkusanyiko, huyu ni mtenda dhambi ambaye amemuasi Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ameenda kinyume na yale ambayo waislamu wameafikiana juu ya kwamba swalah ni katika ´ibaadah bora kabisa. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
“Wanazuoni wameafikiana juu ya kwamba hiyo ni katika ´ibaadah zilizokokotezwa zaidi, utiifu tukufu zaidi na nembo kubwa kabisa ya Uislamu.”[1]
Hata hivyo dhambi hii haimtoi katika Uislamu. Hivyo inafaa kwake akamuoa mwanamke wa Kiislamu ingawa ni bora zaidi kwa mwanamke huyu kuolewa na mwanaume mwingine mwenye dini na maadili mema, ijapo atakuwa na mali kidogo na kabila duni. Kama ilivyopokelewa katika Hadiyth:
“Atakapokujieni yule ambaye mnaridhia dini na tabia yake muozesheni. Msipofanya hivo basi kutakuwa na fitina kubwa na ufisadi wenye kuenea.” Wakasema: “Hata kama hana chochote?” Akasema: “Atakapokujieni yule ambaye mnaridhia dini na tabia yake muozesheni.” Akasema hivo mara tatu[2].
Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanamke anaolewa kwa mambo manne; kwa mali yake, nasaba yake, uzuri wake na kwa dini yake. Hivyo basi mchague yule mwanamke mwenye dini mikono yako ipige mchanga.”[3]
Hadiyth hizi mbili zinafahamisha kuwa dini na maadili mema ndio yanatakiwa yawe mambo yanayozingatiwa na kupatilizwa zaidi kwa mwanamme na mwanamke. Yule msimamizi ambaye anamuogopa Allaah anatakiwa kutilia umuhimu yale aliyoelekeza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu ataulizwa juu ya hilo siku ya Qiyaamah. Allaah (Ta´ala) amesema:
يَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ
”Siku atakapowaita aseme: “Mliwajibu nini Mitume?”[4]
فَلَنَسْأَلَنَّ الَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ وَلَنَسْأَلَنَّ الْمُرْسَلِينَ فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيْهِم بِعِلْمٍ ۖ وَمَا كُنَّا غَائِبِينَ
“Basi bila ya shaka Tutawauliza wale ambao waliopelekewa [Mitume] na tutawauliza Mitume. Kisha Tutawasimulia kwa ujuzi na hatukuwa wenye kukosekana.”[5]
Lakini ikiwa mposaji haswali kabisa, si swalah ya mkusanyiko wala peke yake, huyu ni kafiri aliyetoka katika Uislamu.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (23/222).
[2] at-Tirmidhiy (1085), ambaye amesema kuwa Hadiyth ni nzuri na geni. Nzuri kupitia zingine kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Sunan at-Tirmidhiy” (1085).
[3] al-Bukhaariy (5090) na Muslim (1466).
[4] 28:65
[5] 7:6-7
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/39-41)
- Imechapishwa: 25/03/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/39-41)
Imechapishwa: 25/03/2026
https://firqatunnajia.com/mposaji-haswali/