Mnyama ambaye maumbile yake hana pembe, mkia mdogo au kiziwi katika Udhhiyah

Swali: Ni ipi hukumu ya Udhhiyah au Hadiy ambaye mkia wake ni mdogo au hajaota pembe?

Jibu: Hapana vibaya. Mnyama ambaye hajaota pembe hana neno. Mnyama ambaye mkia wake ni mdogo au hajamea pembe hana neno. Hata hivyo hafai aliyekatika pembe. Kama amekatika pembe yake au mkia wake hasihi. Lakini mnyama hana neno ikiwa maumbile yake kaumbwa hana pembe, kiziwi au mwenye mkia mdogo. Hata hivyo ikiwa mkia wake umekatika, pembe yake imeondoka au imekatika au masikio yamekatika, hapana [hafai].

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1713/حكم-الاضحية-بالبتراء-والجماء
  • Imechapishwa: 15/06/2024