Swali: Mwenye kusema kuwa mlango wa Ijtihaad umefungwa hii leo.

Jibu: Hana khabari. Mlango huo umefungwa kwake yeye na kwa watu mfano wake. Mlango huo umefungwa kwa wajinga. Haukufungwa kwa wanazuoni mpaka pale ambapo Allaah atatuma upepo mzuri uchukue roho za waumini wa kiume na waumini wa kike na kusibaki isipokuwa watu waovu.

Swali: Amesema hivo kwa kuzingatia kutotimia sharti za Mujtahid?

Jibu: Ikiwa sharti hizo hazikutimia kwake basi zimetimia kwa wengine. Ikiwa sharti hizo hazikutimia kwake asifunge mlango.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22011/هل-باب-الاجتهاد-مفتوح-في-هذا-الزمان
  • Imechapishwa: 15/10/2022