Mkutano kati ya Muqbil al-Waadi´iy, raisi wa Yemen na az-Zindaaniy

Watu wengi wamedanganyika na baadhi ya walinganizi. Wanaona hina kwenye ndevu, nguo nusu ya muundi na kilemba kimezungushwa na wanasema “Huyu ni mlinganiaji katika Uislamu”. Nyinyi – majini – lazima pia muwe na aina hii ya watu. Siwezi kuwapa mfano kutoka kwenu, kwa kuwa sijui hali zenu. Nitawapa mfano wa Hizbiyyuun wanaopatikana huku kwetu na jinsi wanavyopotosha maneno.

Mimi na ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy tulikuwa kwa raisi. Nikawaambia:

“Ninawapa changamoto. Mnasema kuwa sisi, Ahl-us-Sunnah, tuna msimamo mkali. Ninawapa changamoto nyote wawili mthibitishe dalili ya kuwa tuko na msimamo mkali.”

Raisi akakaa kimya na apewe honera kwa hilo. Ama ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy, akasema:

“Dalili yangu ni kwamba unazungumzia juu watu.”

Nikamwambia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema kumwambia Mu´aadh:

“Mu´aadh! Wewe ni mtu unayewatia watu katika mtihani”?

Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pia kumwambia Abu Dharr:

“Wewe ni mtu ambaye una chembechembe ya mambo ya kipindi cha kikafiri.”

Raisi akageuka kwa ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy ili apate jibu kwa hilo. ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy akajibu kwa kusema:

“Dalili hizi zimefutwa.”

Nataka hii irekodiwe ili wanachuoni wa waislamu ambao wanawatetea Hizbiyyuun wasikie hili na waone jinsi wanavyohukumu dalili. ´Abdul-Majiyd az-Zindaaniy! Ni nani amesema hili kabla yako? Kasema kuwa dalili hizi zimefutwa. Waulize wanachuoni hata kama ni mwenye kuwafikishwa.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://muqbel.net/sounds.php?sound_id=22
  • Imechapishwa: 10/07/2020