Mke anayeachika kila mwezi

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kumwambia mke wake:

“Wewe ni mwenye kutalikiwa mwanzoni mwa kila mwezi.”?

Jibu: Akimwambia hivo, basi mke huachika kila mwezi unapowadia. Kila mwezi mpya unapoanza, talaka moja inapita. Hadi ukifika mwezi wa tatu, talaka ya tatu inakuwa imeshatimia.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1365/حكم-قول-الرجل-لزوجته-انت-طالق-راس-كل-شهر
  • Imechapishwa: 14/12/2025