Swali: Mwanamke akimkasirikia mumewe kwa sababu ya kidunia, kisha akamkatia mazungumzo na kukaa naye kwa muda fulani unaoendelea kwa siku kadhaa. Ni ipi hukumu ya hilo? Je, kuna neno kuhusu haki za mume juu ya mke wake?
Jibu: Ni wajibu kwa mke kumsikiliza na kumtii mumewe katika mema. Haijuzu kwake kumhama isipokuwa kwa sababu inayokubalika Kishari´ah. Mume pia anapasa kumtendea wema na kutomhama isipokuwa kwa jambo linalokubalika katika Shari´ah. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ
“Na kaeni nao kwa wema.”[1]
وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ
“Nao [wanawake] wana haki kama ambayo [ya waume zao] iliyo juu yao kwa mujibu wa Shari´ah – na wanaume wana daraja zaidi juu yao.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nawausieni kuwatendea wema wanawake.”[3]
[1] 04:19
[2] 02:228
[3] al-Bukhaariy (4787) na Muslim (2671).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/255-256)
- Imechapishwa: 22/02/2026
Swali: Mwanamke akimkasirikia mumewe kwa sababu ya kidunia, kisha akamkatia mazungumzo na kukaa naye kwa muda fulani unaoendelea kwa siku kadhaa. Ni ipi hukumu ya hilo? Je, kuna neno kuhusu haki za mume juu ya mke wake?
Jibu: Ni wajibu kwa mke kumsikiliza na kumtii mumewe katika mema. Haijuzu kwake kumhama isipokuwa kwa sababu inayokubalika Kishari´ah. Mume pia anapasa kumtendea wema na kutomhama isipokuwa kwa jambo linalokubalika katika Shari´ah. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:
وَعَاشِرُوهُنَّ بِالْمَعْرُوفِ
“Na kaeni nao kwa wema.”[1]
وَلَهُنَّ مِثْلُ الَّذِي عَلَيْهِنَّ بِالْمَعْرُوفِ ۚ وَلِلرِّجَالِ عَلَيْهِنَّ دَرَجَةٌ
“Nao [wanawake] wana haki kama ambayo [ya waume zao] iliyo juu yao kwa mujibu wa Shari´ah – na wanaume wana daraja zaidi juu yao.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Nawausieni kuwatendea wema wanawake.”[3]
[1] 04:19
[2] 02:228
[3] al-Bukhaariy (4787) na Muslim (2671).
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/255-256)
Imechapishwa: 22/02/2026
https://firqatunnajia.com/mke-amemsusia-mumewe/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket