Mihraab – Sunnah, ruhusa au inapendeza?

Swali: Ni ipi hukumu ya kutengeneza Mahaarib msikitini?

Jibu: Wanazuoni (Rahimahumu Allaah) wametofautiana juu ya kutengeneza Mihraab kama ni Sunnah, inaruhusu au inapendeza. Vile ninavoona mimi ni kwamba kutengeneza Mihraab ni jambo linaloruhusiwa, maoni ambayo yanayotambulika katika madhehebu ingawa ni vyema pia kwa kusema inapendeza kutokana na yale manufaa mengi yanayopatikana ndani yake ikiwa ni pamoja na kumjuza asiyejua ni wapi kipo Qiblah.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/412)
  • Imechapishwa: 10/04/2026