Swali: Nina dada mwenye umri wa miaka 14, naye amepooza kwa kupooza nusu ya mwili na ana ugumu katika kutia wudhuu´ kwa hali zote. Kwa sababu ya kutoweza kwake, je, inatosha kwake? Je, inafaa kwake Dhuhr pamoja na ´Aswr kwa sababu ya uzito wa kuswali na kusimama ili kuswali katika wakati wake?

Jibu: Aliyepooza, mwanamume au mwanamke, na mgonjwa, mwanamume au mwanamke, Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amebainisha hukumu yao kwa maneno Yake:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

Vilevile hapana vibaya kukusanya swalah mbili katika wakati wa mojawapo yao. Namna yake ni hii: anaweza kuichelewesha swalah ya kwanza mpaka mwisho wa wakati wake na kuisogeza ya pili mwanzo wa wakati wake. Hayo yote yanajuzu kwa udhuru wa Kishari´ah.

Ama kuhusu wudhuu´, ni lazima atawadhe. Ikiwa hawezi kujitawadha mwenyewe, basi wale walio karibu naye wanaweza kumtawadhisha, kama mama yake au dada yake. Wanaweza kumtawadhisha katika sehemu anazoshindwa. Hivyo basi hatakiwi kuacha wudhuu´. Ni sawa kusaidiwa katika wudhuu´. Hakuna ubaya mama yake, dada yake au wengine wakamsaidia kufanya wudhuu´.

[1] 64:16

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/179)
  • Imechapishwa: 09/03/2026