Mgonjwa anatumia dawa baada ya alfajiri kuingia

Swali: Mamangu anameza dawa muda mchache baada ya adhaana ya alfajiri katika Ramadhaan. Mimi nimemzindua ya kwamba akimeza dawa katika wakati kama huu basi bado inamlazimu kufunga siku hiyo.

Jibu: Mgonjwa akimeza dawa katika Ramadhaan baada ya kuingia alfajiri swamw yake si sahihi. Kwa kuwa amekusudia kula. Katika hali hiyo itamlazimu kujizuia na kula na kunywa siku iliyobaki. Isipokuwa ikiwa maradhi yatamuwia magumu. Hapa ndipo itafaa kwake kula kwa sababu ya maradhi na itamlazimu kuilipa siku hiyo. Kwa kuwa amekusudia kula.

Haifai kwa mgonjwa kutumia dawa ilihali amefunga Ramadhaan. Isipokuwa tu wakati wa dharurah. Kwa mfano pale tutapochelea asije kufa. Katika hali hii tutampa dawa ya kumpunguzia. Katika hali hii anakuwa hakufunga. Hakuna dhambi kuacha kufunga kwa sababu ya maradhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/120)
  • Imechapishwa: 07/06/2017