Mgonjwa aliyelisha baada ya kukata tamaa ya kupona analazimika kufunga siku zake akipona?

Swali: Mgonjwa mwenye maradhi yasiyotarajiwa kupona alazimika kufunga au kutoa fidia? Ikiwa analazimika kufidia analazimika kuitanguliza? Anapewa mtu mmoja au watu wengi? Ikitokea akapona ni wajibu kwake kulipa au kulipa kwake kunakuwa kumeanguka?

Jibu: Akipona kutokamana na maradhi sio wajibu kwake kufunga. Kwa sababu ametekeleza wajibu wake na dhimma yake imetakasika. Sentesi nyingine ya swali imeshatangulia kujibiwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (19/123)
  • Imechapishwa: 09/06/2017