Swali: Mimi ni mmoja wa wakufunzi katika chuo cha kijeshi katika mchezo wa karate, ambao ni mchezo wa kujilinda. Chuo hakina sehemu maalum ya mafunzo. Je, inajuzu nifanye mafunzo katika sehemu inayojengwa kwa ajili ya kuwa msikiti lakini bado haijakamilika?

Jibu: Kadiri mafunzo haya yanapokuwa na manufaa katika njia ya Allaah na katika jihaad dhidi ya maadui Zake, basi hapana ubaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaruhusu Wahabeshi kucheza ndani ya msikiti kwa kutumia ngao na mikuki, wakizunguka ndani ya msikiti kwa kutumia silaha hizo. Hivyo basi iwapo mchezo huo unasaidia kujilinda­, kupambana na maadui na kujiepusha na shari zao, hapana tatizo katika kufanya ndani ya msikiti wenye uwazi na nafasi, hadi pale sehemu nyingine itakapopatikana kwa ajili ya mafunzo hayo. Sharti ni kwamba mchezo huo usilete madhara kwa msikiti kwa uharibifu, uchafu au mambo mengine yanayofanana na hayo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30005/هل-يجوز-التدريب-في-مكان-بناء-مسجد
  • Imechapishwa: 26/08/2025