Mayahudi na manaswara waliosikia kuhusu Muhammad lakini wasimwamini

Swali: Watu wa Kitabu waliokuwa wakiishi katika wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wakafa juu ya dini ya ´Iysaa?

Jibu: Ni katika wakazi wa Motoni.

Swali: Walikuwa wakimwabudu Allaah pekee hata hivyo hawakukutana na Uislamu?

Jibu: Waliokufa juu ya dini ya ´Iysaa na Muusa wataingia Peponi. Lakini waliokuwa na Muhammad na wasimwamini wataingia Motoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Naapa kwa yule ambaye nafsi ya Muhammad iko mikononi Mwake. Hatosikia kuhusu mimi sawa awe myahudi au mkristo kisha akafa na asiamini yale niliyotumwa kwayo isipokuwa atakuwa katika watu wa Motoni.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24566/%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%85%D9%86-%D9%85%D8%A7%D8%AA-%D9%86%D8%B5%D8%B1%D8%A7%D9%86%D9%8A%D8%A7-%D9%81%D9%8A-%D8%B2%D9%85%D9%86-%D9%85%D8%AD%D9%85%D8%AF-%EF%B7%BA
  • Imechapishwa: 01/11/2024