Swali: Katika baadhi ya nchi za Kiislamu, kabla imamu hajapanda juu ya mimbari, imekuwa ni ada kwao imamu kutoa mawaidha kwa waswaliji. Je, hilo linajuzu? Je, inajuzu kusoma Suurah Yaa Siyn kwa mtu anayekaribia kufa?
Jibu: Hili halikuwepo katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiingia msikitini anaelekea moja kwa moja kwenye mimbari na kukaa juu yake mpaka muadhini amalize, kisha huanza Khutbah. Hakuwa akiwatolea mawaidha kabla ya hapo. Alipofika (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye mimbari hukaa juu yake, kisha muadhini huadhini na halafu huanza Khutbah. Hivyo ndivyo lililowekwa katika Shari´ah. Ama kuwa anawawaidhi kabla ya hapo, hilo halikuwekwa katika Shari´ah. Bali anaelekea kwenye mimbari na kukaa juu yake, kisha baada ya muadhini kumaliza adhaana ndio anaanza kutoa Khutbah.
Ama kusoma Yaa Siyn kwa mtu anayekaribia kufa, kumepokelewa Hadiyth juu ya hilo, lakini baadhi ya wanazuoni wameifanya dhaifu. Hivyo akisomewa Qur-aan mtu anayekaribia kufa, ni jambo jema.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/255)
- Imechapishwa: 23/02/2026
Swali: Katika baadhi ya nchi za Kiislamu, kabla imamu hajapanda juu ya mimbari, imekuwa ni ada kwao imamu kutoa mawaidha kwa waswaliji. Je, hilo linajuzu? Je, inajuzu kusoma Suurah Yaa Siyn kwa mtu anayekaribia kufa?
Jibu: Hili halikuwepo katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiingia msikitini anaelekea moja kwa moja kwenye mimbari na kukaa juu yake mpaka muadhini amalize, kisha huanza Khutbah. Hakuwa akiwatolea mawaidha kabla ya hapo. Alipofika (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye mimbari hukaa juu yake, kisha muadhini huadhini na halafu huanza Khutbah. Hivyo ndivyo lililowekwa katika Shari´ah. Ama kuwa anawawaidhi kabla ya hapo, hilo halikuwekwa katika Shari´ah. Bali anaelekea kwenye mimbari na kukaa juu yake, kisha baada ya muadhini kumaliza adhaana ndio anaanza kutoa Khutbah.
Ama kusoma Yaa Siyn kwa mtu anayekaribia kufa, kumepokelewa Hadiyth juu ya hilo, lakini baadhi ya wanazuoni wameifanya dhaifu. Hivyo akisomewa Qur-aan mtu anayekaribia kufa, ni jambo jema.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/255)
Imechapishwa: 23/02/2026
https://firqatunnajia.com/mawaidha-siku-ya-ijumaa-kabla-ya-khutbah-ya-ijumaa/
Mshirikishe mwenzako:
- Share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Print (Opens in new window) Print
- Email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Share on X (Opens in new window) X
- Share on Pocket (Opens in new window) Pocket