Maulidi ni kutangulia mbele ya Allaah na Mtume Wake (صلى الله عليه وسلم)

Swali: Ni ipi hukumu ya Shari´ah kwa mtazamo wako kuhusu sikukuu ya kuzaliwa na kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu ni jambo lililoenea kwa wingi huku kwetu?

Jibu: Mtazamo wangu katika masuala haya mimi nasema: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mjumbe kwa viumbe wote na kwamba ni lazima kwa viumbe wote kumwamini na kumfuata yeye. Pamoja na hayo ni lazima kwetu wote kumpenda zaidi kuliko tunavyozipenda nafsi zetu wenyewe, wazazi wetu na watoto wetu. Kwa sababu yeye ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Tunaona kuwa katika kumtukuza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na alama ya kumpenda ni sisi kutomtangulia mbele kwa kitu ambacho hakutuwekea katika Shari´ah. Kwa sababu kufanya hivo kufanya hivo ni kumtangulia mbele yake. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُقَدِّمُوا بَيْنَ يَدَيِ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ سَمِيعٌ عَلِيمٌ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَرْفَعُوا أَصْوَاتَكُمْ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ وَلَا تَجْهَرُوا لَهُ بِالْقَوْلِ كَجَهْرِ بَعْضِكُمْ لِبَعْضٍ أَن تَحْبَطَ أَعْمَالُكُمْ وَأَنتُمْ لَا تَشْعُرُونَ

“Enyi walioamini! Msitangulie mbele ya Allaah na Mtume Wake na mcheni Allaah; hakika Allaah ni Mwenye kusikia yote, Mjuzi wa yote. Enyi walioamini! Msipandishe sauti zenu juu ya sauti ya Nabii na wala msiseme naye kwa sauti ya juu, kama mnavyosemezana wenyewe kwa wenyewe kwa sauti za juu, zisije yakaporomoka matendo yenu nanyi hamhisi.”[1]

[1] 49:01-03

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ajurry.com/vb/showthread.php?t=25122
  • Imechapishwa: 15/11/2019