Matangazo ya mihadhara na darsa msikitini

Swali: Vipi kuhusu kutangaza darsa ndani ya msikiti?

Jibu: Udhahiri ni kwamba hapana vibaya. Hilo sio tangazo. Pia mtu anaweza kusema kwamba jambo hilo linahusiana na msikiti, lakini akiweka tangazo hilo nje ya msikiti itakuwa salama zaidi. Hii ni kwa sababu ya kuenea kwa makatazo ya kuchora au kuandika ndani ya misikiti. Huenda katazo hilo linahusisha pia mambo kama hayo. Isitoshe kwa ajili ya kufunga njia pia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24828/حكم-اعلان-الدروس-والمحاضرات-في-المساجد
  • Imechapishwa: 20/12/2024