Swali: Kuna Hadiyth kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inayosema:
”Msinisifu kwa kupindukia kama manaswara walivomsifu ´Iysaa bwana wa Maryam kwa kupindukia. Hakika si vyengine mimi ni mja wa Allaah.”[1]
Pia kuna Hadiyth nyingine zinazokataza kumsifia au kumtukuza kwa kupindukia mipaka. Lakini wapo watu wanajenga sehemu wanazoita “zawiya,” hukaa humo kwa kufanya Dhikr na nyimbo, hupiga ngoma, hurukaruka, hujiangusha, hujipiga kwa mapanga na viboko, hujichoma moto, hula vioo wakadai kuwa hayo ni matendo yanayowakaribisha kwa Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Je, matendo hayo yana uhusiano wowote na dini khaswa kwa kuzingatia kwamba kuna wasiokuwa waislamu nchini India, China na Japan nao hufanya mambo mfano wake?
Jibu: Hadiyth hiyo ni Swahiyh. Ameipokea al-Bukhaariy katika ”as-Swahiyh” yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Msinisifu kwa kupindukia kama manaswara walivomsifu ´Iysaa bwana wa Maryam kwa kupindukia. Hakika si vyengine mimi ni mja wa Allaah.”
Maana yake ni kwamba hataki kupewa sifa zisizokuwa za haki, kama kudai kuwa anajua ghaibu, akaabudiwa badala ya Allaah, kuwaokoa jamaa zake kutoka Motoni hata wakiwa makafiri na mfano wa hayo.
Mfano wa kupitiliza mipaka ni yale mashairi ya al-Burdah aliposema:
Ee kiumbe mbora! Sina mwengine zaidi yako wa kumkimbilia wakati wa majanga
Usiponitukuza siku ya Qiyaamah na ukanishika mkono, nimeangamia.
Katika ukarimu wako ni pamoja na dunia hii na mali zake
na miongoni mwa elimu zako ni pamoja na elimu ya Ubao na Kalamu
Huku ni kuchupa mipaka kubaya zaidi. Ni kufuru kubwa. Amemfanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa ndiye mwokozi siku ya Qiyaamah, kwamba hakuna kimbilio jengine kwa watu isipokuwa kwake yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwamba anajua ghaibu, kwamba yeye anajua yaliyomo kwenye Ubao na kwenye kalamu na kwamba dunia na Aakhirah ni katika ukarimu wake. Yote haya ni upotofu na kufuru.
Vivyo hivyo kuhusu mwenye kusema juu ya haki ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba yeye anaombwa, kutakwa msaada kwake, wanajikuurbisha kwake kwa vichinjwa na nadhiri, huku ni kuchupa mipaka na ni kusifia kupita mpaka hakujuzu. Bali hiyo ndio shirki kubwa. Haki ya Allaah hapewi mwengine. Haki ya Allaah ni ´ibaadah. Hapewi nayo Mtume wala asiyekuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Ama haya matendo yanayoyafanya Suufiyyah ya kucheza, nyimbo, kujichoma baadhi yao kwa mikuki na mapanga na yaliyofanana na hayo miongoni mwa matendo yao machafu, haya ni Bid´ah walizozizua Suufiyyah. Hayana msingi wowote. Bali ni katika mambo maovu.
Ni wajibu kuyaacha, kuwakataza, kuwaonya kwayo, kutokaa nao na kutowafanya marafiki, kwa kuwa wao wamemzulia Allaah katika hili na wakamdanganya kwa kudai kuwa haya ni dini na kuwa ni ukaribu. Kupiga madufu na nyimbo, kutumia mapanga au visu au mikuki, mashairi yanayopingana na Shari´ah si kutafuta ukaribu kwa Allaah wala utiifu kwa Allaah. Bali haya ni maovu na hayajuzu kwa muislamu kujishughulisha nayo, isipokuwa dufu katika arusi kwa wanawake pekee kwa ajili ya furaha wanapiga wanawake, wasichana wadogo katika ´iyd, kwa kuwa wao ni wadogo, basi wana furaha kama ilivyokuja katika Hadiyth ya ´Aaishah katika kisa cha wasichana wawili waliopiga dufu nyumbani kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku ya ´Iyd. Hili halina tatizo. Limebaguliwa. Lakini waja na wanaume kujishughulisha nayo likiambatana na muziki na nyimbo, ni maovu. Kitendo chote cha Suufiyyah ni maovu, nakusudia hiki ambacho ametaja muulizaji.
Kwa hiyo ni wajibu kujihadhari na haya. Kwa ajili hiyo kwa sababu ya utiifu wao kwa shaytwaan na shaytwaan kushikamana nao, huanguka katika michezo hii, hupatwa na kifafa na shaytwaan akawapambia kwamba haya ni ukaribu na utiifu, kumbe haya ni utiifu wa shaytwaan na ni ´ibaadah ya shaytwaan. Tunamuomba Allaah usalama. Tunamuomba Allaah atuongoze sisi na wao.
[1] al-Bukhaariy (3445), at-Tirmidhiy katika ”ash-Shamaa-il al-Muhammadiyyah” (2/161), ad-Daarimiy (2/230), at-Twayaalisiy (25) na Ahmad (154, 164, 331 na 391).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18148/التحذير-من-الغلو-في-النبي-صلى-الله-عليه-وسلم
- Imechapishwa: 08/09/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/18148/التحذير-من-الغلو-في-النبي-صلى-الله-عليه-وسلم
Imechapishwa: 08/09/2025
https://firqatunnajia.com/matahadharisho-ya-kuchupa-mipaka-kwa-mtume/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket