Swali: Je, inafaa kwa muislamu kumtabania kafiri?

Jibu: Hapana vibaya akimfanyia matabano. Ni kama ambavo anampa dawa. Akiwa ni kafiri anayetangaza amani basi ana haki ya kupewa mkataba. Hata hivyo haifai akiwa ni kafiri anayepiga vita Uislamu. Lakini hapana vibaya akiwa ni kafiri anayetangaza amani na mwenye mkataba. Atabaniwe, kupewa dawa au asaidiwe pesa kidogo akiwa ni fakiri.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24523/هل-يجوز-للمسلم-ان-يرقي-الكافر
  • Imechapishwa: 25/10/2024