Masomo yanawataka wanafunzi wachore viumbe vyenye roho

Swali: Baadhi ya waalimu wanawataka wanafunzi katika baadhi ya masomo wachore picha za viumbe wenye roho au kwa mfano wachore kuku na wanawaambia kukamilisha picha nzima. Wakati mwingine wanawataka vilevile kuichana picha hii au baada ya kupewa picha anataka itiwe rangi kabisa. Ni yapi maoni yako juu ya hili?

Jibu: Naona kuwa ni haramu na ni wajibu kulikataza na kwamba wahusika juu ya masomo wanatakiwa kutekeleza amana katika jambo hili na walikataze. Wanapotaka kuhakikisha akili ya mwanafunzi wanaweza badala yake wakawaambia wachore picha ya gari, mti na mfano wa hayo katika mambo yanayoizunguka elimu yake. Kwa hivyo itapata kujulikana akili ya mwanafunzi huyu na kuyatekeleza kwake mambo.

Haya ni katika mambo ambayo watu wamepewa mtihani kwayo kupitia shaytwaan. Vinginevyo hapana shaka katika mtu kuhakikisha umairi wake wa kuchora baina ya kuchora picha ya mti, gari, kasiri na kuchora mtu. Naona kuwa ni wajibu kwa wahusika kukataza jambo hili. Mwanafunzi akipewa mtihani na akawa analazimika kuchora basi achore mnyama asiyekuwa na kichwa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/273-274)
  • Imechapishwa: 02/07/2017