Swali: Je, ni sahihi kukusanya nia mbili wakati mtu anafunga siku moja, kwa mfano mtu akafunga moja katika zile siku sita pamoja na siku moja katika yale masiku Meupe?
Jibu: Wakati fulani ´ibaadah moja inadondosha nyingine. Kutokana na ninavojua ni kwamba malengo ya ´ibaadah hiyo yanatimia katika wakati huo pasi na kuzingatia ´ibaadah yenyewe. Kwa mfano mtu akiingia msikitini hatakiwi kuketi chini mpaka kwanza aswali Rak´ah mbili. Akiingia msikitini na akaswali Sunnah ya Raatibah, basi inadondoka zile Rak´ah mbili za mamkuzi ya msikiti. Kwa sababu malengo ni kwamba asiketi chini mpaka kwanza aswali, jambo ambalo ameshalifanya. Vivyo hivyo mtu akiingia msikitini na akamkuta imamu anaswali; atajiunga na imamu na hatokuwa na haja ya kuswali Rak´ah mbili zinazoswaliwa kwa ajili ya mamkuzi ya msikiti.
Vivyo hivyo mtu akifunga yale masiku sita ya Shawwaal. Masiku hayo yanafunika yale masiku Meupe. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifunga masiku matatu katika kila mwezi na wala hajali ameyafunga mwanzoni mwa mwezi, katikati yake au mwishoni mwake.”[1]
Lakini ikiwa unataka kufunga masiku Meupe, basi funga masiku siku ya Shawwaal mwanzoni mwa mwezi na yakifika masiku Meupe utayafunga. Hata hivyo masiku sita ya Shawwaal yanatosheleza kutokana na kufunga siku tatu.
[1] Muslim (1160).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/14-15)
- Imechapishwa: 31/03/2026
Swali: Je, ni sahihi kukusanya nia mbili wakati mtu anafunga siku moja, kwa mfano mtu akafunga moja katika zile siku sita pamoja na siku moja katika yale masiku Meupe?
Jibu: Wakati fulani ´ibaadah moja inadondosha nyingine. Kutokana na ninavojua ni kwamba malengo ya ´ibaadah hiyo yanatimia katika wakati huo pasi na kuzingatia ´ibaadah yenyewe. Kwa mfano mtu akiingia msikitini hatakiwi kuketi chini mpaka kwanza aswali Rak´ah mbili. Akiingia msikitini na akaswali Sunnah ya Raatibah, basi inadondoka zile Rak´ah mbili za mamkuzi ya msikiti. Kwa sababu malengo ni kwamba asiketi chini mpaka kwanza aswali, jambo ambalo ameshalifanya. Vivyo hivyo mtu akiingia msikitini na akamkuta imamu anaswali; atajiunga na imamu na hatokuwa na haja ya kuswali Rak´ah mbili zinazoswaliwa kwa ajili ya mamkuzi ya msikiti.
Vivyo hivyo mtu akifunga yale masiku sita ya Shawwaal. Masiku hayo yanafunika yale masiku Meupe. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifunga masiku matatu katika kila mwezi na wala hajali ameyafunga mwanzoni mwa mwezi, katikati yake au mwishoni mwake.”[1]
Lakini ikiwa unataka kufunga masiku Meupe, basi funga masiku siku ya Shawwaal mwanzoni mwa mwezi na yakifika masiku Meupe utayafunga. Hata hivyo masiku sita ya Shawwaal yanatosheleza kutokana na kufunga siku tatu.
[1] Muslim (1160).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (20/14-15)
Imechapishwa: 31/03/2026
https://firqatunnajia.com/masiku-sita-ya-shawwaal-yanatosheleza-kutokana-na-yale-masiku-meupe/