Mara inanyanyuliwa na mara hainyanyuliwi

Swali: Wako wanazuoni wanaosema kuwa kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa ni miongoni mwa sababu za kukubaliwa du´aa. Lakini tumesikia fatwa ukisema kwamba haifai kunyanyua mikono wakati wa kuomba du´aa.

Jibu: Si kila du´aa mtu ananyanyua mikono. Mara hunyanyuliwa na mara nyingine hainyanyuliwi. Baada ya swalah za faradhi haikupokelewa kuwa mikono inanyanyuliwa. Baada ya adhaana vivyo hivyo. Baada ya swalah za faradhi haikupokelewa kuwa mikono inanyanyuliwa. Aombe du´aa lakini pasi na kunyanyua mikono. Sisi tunafuata dalili; zile hali ambazo imepokelewa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amenyanyua mikono nasi tunanyanyua mikono yetu. Khutbah ya ijumaa mtu aitikie du´aa bila ya kunyanyua mikono, ni kitu kisichojuzu na ni Bid´ah. Isipokuwa Khatwiyb akiomba du´aa ya kunyesha mvua ndio mtu anyanyue mikono.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (27)
  • Imechapishwa: 15/04/2021