Mapenzi ya asiyekuwa Allaah na Mtume yanayopelekea katika shirki

Swali 64: Vipi kuhusu mtu ambaye Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si wenye kupendwa zaidi kwake?

Jibu: Mwenye kupendelea uzinifu na wizi, lakini hakuna anayempenda zaidi kuliko Allaah na Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi huyo si kafiri. Hata hivyo ikiwa anawapenda wasiokuwa wawili hao mapenzi ya ´ibaadah, amekufuru na kufanya shirki. Mapenzi aina hiyo yamemwingiza ndani ya shirki, kama ilivyo hali ya waabudu makaburi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 45
  • Imechapishwa: 08/08/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´