Swali: Maoni ya wanazuoni yametofautiana kuhusu hukumu ya zakaah ya mapambo ya dhahabu yanayotumika na yasiyotumika. Ni yepi maoni yenu katika suala hili?
Jibu: Maoni yenye nguvu ni kwamba mapambo ya wanawake, ni mamoja iwe yanatumika au hayatumiki, yanapaswa kutolewa zakaah endapo yatakuwa yametimia mwaka na yakafikia kiwango kinachotakiwa kutolewa zakaah. Hii ni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamuru mwanamke mwenye mapambo atoe zakaah yake. Umm Salamah alipomwonyesha mapambo yake, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
”Kile kiwango kilichofikia kutolewa zakaah kikatolewa zakaah, basi sio kulimbikiza.”
Akamwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yule mwanamke aliyekuwa na bangili mbili ambazo hazitozwi zakaah:
”Je, unafurahia Allaah akuvishe bangili mbili za Moto kutokana nazo?”
Kwa hiyo ni wajibu kwa mwanamke mwenye mapambo anayoyavaa au asiyoyavaa kuyatolea zakaah pindi yanapotimia mwaka na kufikia kile kiwango kinachotakiwa kutolewa zakaah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31768/ما-الراجح-في-زكاة-الحلي-المستعمل
- Imechapishwa: 30/11/2025
Swali: Maoni ya wanazuoni yametofautiana kuhusu hukumu ya zakaah ya mapambo ya dhahabu yanayotumika na yasiyotumika. Ni yepi maoni yenu katika suala hili?
Jibu: Maoni yenye nguvu ni kwamba mapambo ya wanawake, ni mamoja iwe yanatumika au hayatumiki, yanapaswa kutolewa zakaah endapo yatakuwa yametimia mwaka na yakafikia kiwango kinachotakiwa kutolewa zakaah. Hii ni kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamuru mwanamke mwenye mapambo atoe zakaah yake. Umm Salamah alipomwonyesha mapambo yake, Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:
”Kile kiwango kilichofikia kutolewa zakaah kikatolewa zakaah, basi sio kulimbikiza.”
Akamwambia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yule mwanamke aliyekuwa na bangili mbili ambazo hazitozwi zakaah:
”Je, unafurahia Allaah akuvishe bangili mbili za Moto kutokana nazo?”
Kwa hiyo ni wajibu kwa mwanamke mwenye mapambo anayoyavaa au asiyoyavaa kuyatolea zakaah pindi yanapotimia mwaka na kufikia kile kiwango kinachotakiwa kutolewa zakaah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31768/ما-الراجح-في-زكاة-الحلي-المستعمل
Imechapishwa: 30/11/2025
https://firqatunnajia.com/maoni-yenye-nguvu-kuhusu-mapambo-ya-wanawake-ya-dhahabu-na-fedha/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket