Manii yanamtoka kwa siku mara kadhaa bila ya shahawa

Swali: Kuna ndugu mwenye hali ya ugonjwa ambapo manii humtoka mara nyingi kwa siku. Wakati mwingine kwa shahawa na wakati mwingine pasi na shahawa. Huenda hali hiyo ikamtokea akiwa msikitini. Ni ipi hukumu ya hali hii?

Jibu: Ikiwa manii yamemtoka kwa shahawa, basi ni lazima atoke msikitini ikiwa jambo hilo limemtokea ndani yake na aoge janaba. Ikiwa manii yamemtoka bila shahawa, si lazima atoke msikitini wala kuoga janaba. Bali anatakiwa kutawadha kwa sababu ya hilo wakati wa kila swalah, baada ya kufanya kujisafisha na maji. Pia anatakiwa kuuhifadhi msikiti usichafuliwe na yale yanayotoka kwake akiwa msikitini.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/322)
  • Imechapishwa: 20/11/2026