Swali: Je, manii ni kitu kisafi au najisi? Je, inatosha kuyakwangura yakikauka na kuyaosha ikiwa bado ni mabichi?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba manii ni kitu kilicho katika hali ya usafi. Manii ndiyo msingi wa mtu. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anhaa) amesema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wakati mwingine alikuwa anaosha manii, na wakati mwingine alikuwa anayakwangura tu yakiwa yamekauka. Amesema:

“Nilikuwa nayakwangura yakiwa makavu kutoka kwenye nguo yake.”

Hii inaonyesha kuwa manii ni kitu kisicho najisi. Lau yangekuwa najisi, basi yangelazimu kuoshwa. Jengine ni kwamba manii ndio msingi wa mtu. Mtu ni msafi na asili yake ni msafi. Msingi wake ni udongo na udongo ni msafi. Isitoshe manii ni kitu kisafi na hivyo mwanadamu ni msafi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1183/هل-المني-طاهر-ام-نجس
  • Imechapishwa: 07/02/2026