Mama mkwe kujifunua mbele ya mkwe wake baada ya talaka

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kujifunua mbele ya mume wa msichana wake baada ya msichana huyo kuachika na mwanaume huyo?

Jibu: Ndio, ni Mahram kwake hata kama binti yake amekufa au ametalikiwa. Mume wa binti na mume wa mama ni Mahram, hata kama mama amekufa, msichana amekufa au ameachika. Hivyo basi mume wa binti ni Mahram kwake. Allaah amesema:

حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ أُمَّهَاتُكُمْ وَبَنَاتُكُمْ وَأَخَوَاتُكُمْ وَعَمَّاتُكُمْ وَخَالَاتُكُمْ وَبَنَاتُ الْأَخِ وَبَنَاتُ الْأُخْتِ وَأُمَّهَاتُكُمُ اللَّاتِي أَرْضَعْنَكُمْ وَأَخَوَاتُكُم مِّنَ الرَّضَاعَةِ وَأُمَّهَاتُ نِسَائِكُمْ

“Mmeharamishiwa [kuwaoa] mama zenu na wasichana wenu na dada zenu na shangazi zenu na makhalati wenu na wasichana wa kaka na wasichana wa dada na mama zenu ambao wamekunyonyesheni na ndugu zenu kwa kunyonya na mama wa wake zenu… “ (04:23)

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30953/هل-تظل-المراة-محرما-لزوج-ابنتها-بعد-الطلاق
  • Imechapishwa: 17/09/2025