Kuna biashara ambayo watu wengi wanafanya na ambayo pia inajuzishwa na wanazuoni wengi, nayo ni malipo ya awamu. Malipo ya malipo yanamaanisha kuwa muuzaji anakuambia kuwa unaweza kununua bidhaa kwa 20.000 kwa mkopo au 17,000 taslimu. Hii ndio maana ya ribaa. Abu Daawuud amepokea kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amekataza biashara mbili katika biashara moja ambapo baadhi waliona wanalazimika kufasiri Hadiyth hii kwa njia ya kwamba biashara moja ni sahihi na biashara nyingine siyo sahihi. Wengine pia wanasema kwamba Hadiyth inahusu biashara inayoelea ambayo sio ya uhakika. Kwa hali yoyote nasema kwamba ununuzi kama huo una maana ya ribaa.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 280-281
  • Imechapishwa: 16/04/2025