Mali unayotakiwa kuikubali na kuikataa

Ikiwa mali imekufikia kwa njia inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah, basi ichukue wala usiikatae. Ukipenda uitumie kwa ajili yako mwenyewe, au ukapenda uitoe kama swadaqah au uitumie katika mradi wa kheri, yote hayo yanafaa. Lakini ikiwa mali hiyo imekujia kwa njia isiyokubalika katika Shari´ah, kama kupitia rushwa, wizi au kuwadhulumu watu, basi usiipokee na wala usisaidie katika kumuasi Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2209/شرح-حديث-وما-جاءك-من-هذا-المال-وانت-غير-مشرف
  • Imechapishwa: 03/01/2026