Swali: Maneno ya ash-Shaafi’iy (Rahimahu Allaah):
”Akijifunza uchawi tutamwambia atueleze uchawi wake.” Akitueleze yale yanayopelekea katika ukafiri kama vile imani ya watu wa Babeli ya kujikurubisha kwa nyota saba na kwamba anafanya kile wanachotaka, basi ni kafiri. Na ikiwa mambo hayo hayapelekei katika kufuru, akiona kufaa kwake, anakufuru.”
Jibu: Maana yake ni kwamba baadhi ya watu hawaelewi uchawi ni kitu gani. Wakifahamishwa kwamba uchawi ni kule kuwategemea mashaytwaan, kuwaomba badala ya Allaah, kuyaomba masanamu au mizimu, basi hiyo ni shirki kubwa na janga kubwa. Lakini ikiwa ni dawa anazotengeneza au kitu kinachowadhuru watu hakiitwi kuwa ni uchawi. Kitu ambacho hakihusiani na kumwabudu mwengine asiyekuwa Allaah wala hakiwaathiri hakiitwi kuwa ni uchawi. Hakika hapana vyenginevyo ni mambo tu yanayowadhuru watu kama vile maradhi na madonda. Haya ndio makusudio yake. Jambo ambalo halihusiani na kumwabudu mwengine asiyekuwa Allaah. Anaweza kutumia kitu kinachowadhuru watu, lakini hata hivyo sio uchawi. Kinawadhuru kwenye miguu, mikono na vichwa vyao. Ni vitu wanavyotumia kama vile wanja, mafuta au vyenginevyo vinavyowadhuru ambavyo havihusiani na kumwabudu mwengine asiyekuwa Allaah. Hiyo ni dhuluma na uadui na sio uchawi wala ukuhani.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24607/ما-وصف-السحر-الذي-يوصف-بالكفر-فاعله
- Imechapishwa: 17/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)