Swali: Iwapo muislamu atashika njia ya kutafuta elimu isiyokuwa ya dini – kama vile udaktari au uhandisi – Je, anaingia ndani ya Hadiyth[1]?

Jibu: Maoni ya karibu zaidi na usahihi – na Allaah ndiye anayejua zaidi – ni kwamba kinachokusudiwa ni elimu ya kidini. Kuhusu elimu nyingine zinaruhusiwa. Muda wa kuwa amekusudia kheri, basi kunatarajiwa kwake kheri. Ikiwa amekusudia nazo kuwanufaisha waislamu, kama vile udaktari, uhandisi au hesabu, na akakusudia kwazo kuwanufaisha waislamu, basi kunatarajiwa kwake kheri – Allaah akitaka. Lakini neno elimu linapotajwa kwa kuachiliwa, basi kunakusudiwa elimu ya yale aliyosema Allaah na Mtume wake. Hiyo ndio elimu.

[1] Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yeyote mwenye kushika njia akitafuta kwayo elimu, basi Allaah atamsahilishia njia ya kuelekea Peponi.” (Muslim (2699))

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25200/من-سلك-طريقا-يلتمس-فيه-علما-هل-يشمل-العلم-الدنيوي
  • Imechapishwa: 14/02/2025