Makatazo ya kufunga mwaka mzima na kuhusu Maswahabah waliounganisha swawm

Swali: Kuna masimulizi yamepokelewa kutoka kwa ´Umar, kutoka kwa ´Aaishah na kutoka kwa Abu Twalhah aliyopokea at-Twabaraaniy, Abu Bakr al-Firyaabiy na Ibn Sa´d, ya kwamba walikuwa wakiunganisha swawm na baadhi ya wengine walikuwa wakifunga mwaka mzima. Ni vipi yanafasiriwa mapokezi haya?

Jibu: Aliyezitaja dalili zimechikana kwake. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amekataza kuunganisha swawm na kufunga mwaka mzima na akasema kuwa hafunga ambaye amefunga mwaka mzima. Wale Maswahabah waliofanya hivo Sunnah ilijificha kwao. Sunnah ndio yenye kuamua kati ya watu:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

”Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume.”[1]

Hakusema lirudishwe kwa Zayd wala ´Amr.

Swali: Makatazo ya kuunganisha swawm ni jambo ambalo limetangaa?

Jibu: Vyovyote vile mtu afuate Sunnah na si Zayd wal ´Amr. Ajitahidi kufuata Sunnah. Ikiwa anataka kufunga basi ni vyema afunge siku moja na kufungua siku ya kufuatia, afunge jumatatu na alkhamisi na siku tatu za kila mwezi. Ama kufululiza swawm mwaka mzima si sawa. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema juu ya mtu huyo:

”Hafunga na wala hakufungua.”

Hakufunga ambaye amefunga milele. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amekataza hilo. Wakati Maswahabah walipomuomba kuunganisha swawm akaunganisha nao funga siku moja, kisha siku nyingine, kisha akasema wakati alipoona mwezi mwandamo:

”Kama ungelichelewa basi ningekuzidishieni.”

Alisema hivo kwa njia ya makemeo baada ya kuwakataza lakini wakang´ang´ania.

[1] 04:59

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24647/علام-يحمل-سرد-بعض-الصحابة-الصوم
  • Imechapishwa: 18/11/2024