Swali: Jioni moja Ramadhaan nilipokuwa nimefunga nikaingia bafuni kwa ajili ya kutawadha. Nilikuwa na mazowea pindi ninapomaliza kukojoa basi najikamua ili kusibaki mkojo wowote. Nilipomaliza kukojoa nikatokwa na majimaji kwenye tupu yangu yanayofanana kama manii. Lakini hata hivyo majimaji haya yakatoka bila ya kuhisi matamanio kama ya manii. Nikaendelea na swawm yangu mpaka wakati wa maghrib. Je, kutokwa na majimaji haya yanaiathiri swawm yangu? Je, majimaji haya yanamuwajibisha mtu kuoga au hapana? Ikiwa nalazimika kuilipa siku hii lakini hata hivyo sikuilipa isipokuwa baada ya kupita Ramadhaan ya pili ni kipi kinachonilazimu?
Jibu: Kutokwa na majimaji ambayo ni mazito kiasi baada ya kukojoa sio manii. Hayo ni wadiy. Hayaiharibu swawm na wala hayamuwajibishi mtu kuoga. Yanachowajibisha ni kuosha kwa maji na kutawadha. Midhali hukukata swawm yako na wala hukunuia kuikata kabla ya kufika maghrib basi swawm yako ni sahihi na wala huhitajii kuilipa.
- Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/280)
- Imechapishwa: 11/06/2017
Swali: Jioni moja Ramadhaan nilipokuwa nimefunga nikaingia bafuni kwa ajili ya kutawadha. Nilikuwa na mazowea pindi ninapomaliza kukojoa basi najikamua ili kusibaki mkojo wowote. Nilipomaliza kukojoa nikatokwa na majimaji kwenye tupu yangu yanayofanana kama manii. Lakini hata hivyo majimaji haya yakatoka bila ya kuhisi matamanio kama ya manii. Nikaendelea na swawm yangu mpaka wakati wa maghrib. Je, kutokwa na majimaji haya yanaiathiri swawm yangu? Je, majimaji haya yanamuwajibisha mtu kuoga au hapana? Ikiwa nalazimika kuilipa siku hii lakini hata hivyo sikuilipa isipokuwa baada ya kupita Ramadhaan ya pili ni kipi kinachonilazimu?
Jibu: Kutokwa na majimaji ambayo ni mazito kiasi baada ya kukojoa sio manii. Hayo ni wadiy. Hayaiharibu swawm na wala hayamuwajibishi mtu kuoga. Yanachowajibisha ni kuosha kwa maji na kutawadha. Midhali hukukata swawm yako na wala hukunuia kuikata kabla ya kufika maghrib basi swawm yako ni sahihi na wala huhitajii kuilipa.
Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/280)
Imechapishwa: 11/06/2017
https://firqatunnajia.com/majimaji-mazito-yanayotoka-baada-ya-kukojoa-yanaharibu-swawm/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)