Maji ya kidinbwi ambayo yanachanganyika na majani

Swali: Tulitoka kundi kwenda porini ambapo tukakaa karibu na kidimbwi cha maji na maji yalikuwa yamechanganyika na matope na baadhi ya majani. Je, inajuzu kutawadha kwa maji hayo kwa ajili ya swalah?

Jibu: Inajuzu kutawadha kwa maji kama hayo, kuoga kwa maji hayo na hata kunywa maji hayo, kwa sababu bado yana jina lake la ´maji`. Hivyo ni maji masafi. Yale yaliyoyachanganyika nayo kama udongo na majani hayaliondoi sifa yake ya kuwa ni masafi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/17)
  • Imechapishwa: 19/02/2026