Mahari na eda ya mwanamke ambaye mumewe amekufa kabla ya tendo la ndoa

Swali: Je, mke atamrithi mume wake ikiwa atafariki kabla ya kumjamii? Je, atakaa eda na atapata mahari?

Jibu: Ndio, ikiwa amefunga ndoa naye kisha akafariki kabla ya kumwingilia, basi atamrithi. Mwanamke huyo yuko na eda, ana haki ya mirathi na mahari aliyomtajia. Ikiwa hakumtajia mahari, basi atapewa mfano wa mahari ya wanawake wa ukoo wake, kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Ma´qil bin Sinaan al-Ashja´iy. Vilevile Ibn Mas´uud alitoa fatwa kwa hilo. Hivyo basi mume akifariki kabla ya kumwingilia na kabla ya kumtajia mahari, basi atapewa mfano wa mahari ya wanawake wa ukoo wake, bila kupunguziwa wala kuzidishiwa. Aidha atakaa eda na ana haki ya mirathi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30080/ما-عدة-وميراث-من-توفي-زوجها-قبل-الدخول
  • Imechapishwa: 06/09/2025