Mafukara wa nchi wana haki zaidi ya zakaah

Swali: Je, inafaa kutoa pesa za zakaah, swadaqah na kafara kwa waislamu mafukara walioko nje ya nchi au ni lazima kuitoa kwa mafukara walioko ndani ya nchi?

Jibu: Imepokelewa katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) katika khabari inayosema kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwagiza Mu´aadh kwenda Yemen na kwamba alimwamrisha baadhi ya mambo ikiwa ni pamoja na:

“… wajulishe kuwa Allaah amefaradhisha juu yao zakaah katika mali yao ambayo itachukuliwa kutoka kwa wale matajiri wao na watapewa mafukara wao.”[1]

Zakaah wanapewa wakazi wa nchi. Wakitoshelezwa basi itafaa kuipeleka katika nchi zingine.

[1] al-Bukhaariy (1395), Muslim (19) na wengineo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/الزكاة-للداخل-أم-للخارج
  • Imechapishwa: 12/06/2022