Mabaki ya manii yanayotoka baada ya josho la janaba

Swali: Mtu alimjamiiana mke wake, kisha akaoga josho la janaba. Baada ya hapo mabaki ya manii yakatoka pamoja na mkojo. Je, anatakiwa kurudia josho?

Jibu: Yule aliyeoga josho la janaba, kisha manii yakatoka baada ya josho hilo, josho lake linamtosheleza na si wajibu kwake kulirudia. Bali ni wajibu kwake kujisafisha kwa maji na kutawadha.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/300)
  • Imechapishwa: 14/11/2026