Swali: Ni nini maana ya ushahidi wa uwongo (قول الزور)?

Jibu: Uwongo.

Mwanafunzi: Uwongo tu?

Ibn Baaz:  Ushahidi wa uwongo ni uwongo.

Swali: Je, ndani yake hakuingii kitu katika yaliyoharamishwa?

Ibn Baaz: Ushahidi wa uwongo ni tofauti na kutenda yaliyoharamishwa, kwani huko ni kule kuyafanyia kazi.

Mwanafunzi: Vipi kuhusu kuyafanyia kazi?

Ibn Baaz: Kufanyia kazi ni kule kuyatenda yaliyoharamishwa. Kwa kuwa mtu anadai imani, lakini yuko na kitu katika uwongo kwa namna ya kuyatenda yaliyoharamishwa ambayo yanaipunguza na kudhoofisha imani yake. Maasi yote yanadhoofisha imani.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30887/ما-معنى-قول-الزور-والعمل-به
  • Imechapishwa: 14/09/2025